Deuteronomy 6:14-19

14Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; 15 akwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi. 16 bUsimjaribu Bwana Mwenyezi Mungu wako kama ulivyofanya huko Masa. 17 cUtayashika maagizo ya Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa. 18 dFanya lililo haki na jema mbele za Bwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zako, 19 ekuwafukuza kwa nguvu adui zako mbele yako kama Bwana alivyosema.

Copyright information for SwhKC